Dar es salaam likiwa jiji la tisa kwa ukuaji duniani huku kwa Afrika likishika nafasi ya tatu, limekua na foleni kubwa ambazo mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inasema huwa kila siku inapatikana hasara ya shilingi BILIONI TATU kutokana na foleni Dar es salaam.
Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’
Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.
Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.
credit: Milladiayo
No Comment to " Treni za juu kama hizi kujengwa Dar hivi karibuni. Serikali yathibitisha. "