Mkuu wa usalama barabarani Vale Manga Wilma amesema aina hii ya taa za Robot imesaidia kupunguza msongamano na kuleta urahisi ambao haukuwepo mwanzoni.
Robot hizi zinatumia umeme wa jua ambapo huwa zinafanya kazi saa 24 huku zikiwa na camera pia ili kurekodi kila tukio ikiwemo mwenendo wa magari.
Robot hizi pia zimewezeshwa kuweza kufanya baadhi ya vitu kama binadamu au kama askari wa usalama barabarani anavyofanya ikiwemo kunyanyua mkono kuongoza magari na kutoa sauti (kuongea) kwenye kuvusha watu.
Kingine kizuri ni kwamba hizi taa zimetengenezwa na Mainjinia wa hapohapo Congo DRC waitwao WITECH ONG.
Koment chini.
No Comment to " Tazama Picha 7 za aina ya taa zinazotumika kuongozea magari Kinshasa Congo DRC. Na sisi je? "