.

MWALIMU MKUU MATATANI: KANDA YA NGONO YAMPONZA, ATIMULIWA KAZI. Tazama hapa

By Unknown - Friday, 9 May 2014 No Comments
Mwalimu mkuu wa shule moja ya upili nchini Uingereza ameachishwa kazi kufuatia utata kuhusu kanda ya ngono inayodaiwa kurekodiwa shuleni humo.
Shule iliyokumbwa na kashfa
Mwenyekiti wa bodi ya shule alimwachisha kazi mwa muda mwalimu mkuu Graham Daniels na mfanyakazi mwingine wa shule ambaye jina lake halikutajwa baada ya malalamiko kutolewa kuwahusu wawili hao
Kuachishwa kazi kwa mwalimu huyo kulitokea baada ya wanafunzi kusambaza kanda hiyo kwa mitandao ya kijamii. Kanda hiyo ilikuwa na sauti za watu wawili wakijihusisha na ngono katika chumba kimoja cha shule hiyo.
Hata hivyo wakuu wa bodi walisema kuwa shughuli za masomo zinaendelea kama kawaida.
Mkuu wa bodi alisema: "shule imepokea malalamiko ambayo hayakumtaja mtu yeyote lakini kufuatia madai hayo uchunguzi utafanywa.''
Mwalimu mkuu na mfanyakazi mwingine wa shule wameachishwa kazi kutokana na madai hayo.

SOURCE: BBC

No Comment to " MWALIMU MKUU MATATANI: KANDA YA NGONO YAMPONZA, ATIMULIWA KAZI. Tazama hapa "

­