Hii stori ilianza baada ya kutoka kwa jarida la Vibe Magazine ambalo lilitoka wiki iliyopita,mbele ya jarida hilo kulikua na picha ya Ommy Dimpoz akiwa kakaa huku miguu akionekana na mavazi ya kike,mjadala huu ulianza baada ya kuonekana kwa viatu hivyo na wengine wakidai kuwa hata suruali haikua ya kiume.
Ommy Dimpoz aliongea na Dj Fetty kupitia So so Fresh ya Ijumaa mei 09,hiki ndicho alichokisema>>’Viatu sio vya kike kwa sababuukisema viatu vya kike unamaanisha labda umeenda kununua kwenye duka la vitu vya kike na viatu vile mimi nimenunua South Africa kipindi tumeenda kumsindikiza AY kwenye Channel O’
‘Nakumbuka tena siku ambayo nimeenda kununua nilikuwa na Dulla Spatan nilinunua kama jozi ishirini au thelethini zilikuwa jozi nyingi unajua muda mwingine unaweza kuingia kwenye maduka ukakuta kuna vitu vinauzwa,kwahiyo nilikuta,halafu na vile vilikuwa ni vyepesi havina uzito’
‘kwahiyo nikanunua nunua vile vingi,lakini nimenunua kwenye Mr Price nakumbuka, vilikuwa ni rahisi,sidhani kama watu wameichukuliaje lakini huenda labda fashion ndio imenigharimu,lakini naona ni viatu vya kawaida na watu wanavaa hata ukiangalia wanamitindo’
‘Hata watu wengi wanavaa kwahiyo kwa kununua mi nimenunua sehemu ya vitu vya kiume na hakikua kimoja kusema labda wamekosea wamekiweka sehem tofauti, ni kwamba viko vingi na aina tofauti’.
Hapa ipo interview yake aliyofanya na Dj Fetty.
No Comment to " Sikiliza Kauli ya Ommy Dimpoz baada ya tuhuma za kuvaa viatu vya kike. Vitazame viat halafu sema neno "